BONGO MUVI WACHAFUKWA!

Na: Gladness Mallya na Imelda Mtema
JAMBO limezua jambo! Baada ya hivi karibuni wasanii wa Bongo Muvi (Movie) kufanya dua kwa ajili ya wenzao waliofariki dunia, baadhi ya ndugu wa marehemu wamecharuka na kudai kuwa waandaaji wa kisomo hicho walifanya kwa manufaa yao binafsi.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa marehemu wanalalamika kuwa dua hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar, ilikuwa ni kwa ajili ya kujipatia fedha yeye ndiyo maana hakuona haja ya kuwashirikisha.
“Dua ilifanyika lakini baadhi ya ndugu wa marehemu hawakuambiwa na wanalalamikia sana kitendo hicho kwani si cha kiungwana, kimsingi mamilioni waliyopewa na mdhamini wa shughuli yametumika vibaya,” kilidai chanzo hicho bila kueleza fedha hizo zimepatikana wapi.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza jambo.
Baada ya malalamiko hayo kutua mezani, mapaparazi wetu waliwatafuta ndugu wa marehemu ambao hawakuonekana kwenye dua hiyo ambapo walifunguka kwa nyakati tofauti:
MKE WA MZEE SMALL
Bi. Fatuma Said ambaye ni mke wa aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ alisema kwamba hawakupewa taarifa wao kama familia jambo ambalo limemsikitisha sana.
Aliyekuwa mke wa muongozaji wa filamu Bongo(George Otieno Tyson) Beatrice Shayo.
“Imeniuma kwa kweli kwani sisi wajane tunatengwa sana, yaani wasanii wakishazika hakuna anayerudi nyuma tena, kitendo cha kutokututaarifu kuhusu dua kimeniumiza sana jamani tungepewa tu taarifa,” alisema Fatuma.
BEATRICE SHAYO ‘MKE WA TYSON’
Huyu ni mwanadada aliyekuwa mke wa marehemu, George Otieno ‘Tyson’ ambaye naye alikiri kwamba hakuwepo kwenye dua kwa sababu hakuwa na taarifa.
Aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ enzi za uhai wake.
“Sikujisikia vizuri na imeniuma sana kwani sikujua inafanyika wapi na imeandaliwa na nani, ukweli walioandaa hawakufanya vizuri kwani walipaswa kutushirikisha sisi wahusika ili tuwe kitu kimoja, sasa nashangaa walifanyaje dua wakati ndugu na jamaa wa marehemu hawana taarifa?” alisema Beatrice.
MAMA SHARO
Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ ambaye alisema kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu dua na ndiyo alisikia kutoka kwa mwandishi.
“Ndiyo nasikia kwako, ukweli nimeumia kutokupewa taarifa kwani ningejumuika na mimi kwa ajili ya kumuombea mwanangu, naona wamenitupa na kunisahau kabisa, wasanii msiwe mnanitenga hivyo jamani!” alisema Mama Sharo.
Aliyekuwa mkongwe wa maigizo nchini, marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ enzi za uhai wake.
SETH BOSCO
Ni mdogo wa marehemu Steven Kanumba ambaye alitafutwa baada ya simu ya mama Kanumba kuita bila kupokelewa ambapo alisema wao kama familia hawakupewa taarifa ndiyo maana hawakuonekana kwenye dua hiyo jambo ambalo limewahuzunisha.
“Aliyeandaa dua hiyo hakufanya jambo la kiungwana, tumejisikia vibaya sana kwani suala kama hilo walitakiwa kuwafuata wahusika na kuwaalika tena ikiwezekana washirikiane kwa pamoja lakini walifanya kwa ajili ya kujipatia fedha tu hakuna chochote,” alisema Seth.
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
MSIKILIZE RAIS
Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba alilaani vikali kitendo hicho na kusema waandaaji hawakufuata utaratibu.
“Walitakiwa kuwashirikisha wahusika na mazingira haya tata ndiyo maana maswali yanakuwa mengi vinywani mwa watu kwamba hakikuwa kitu chema na cha uungwana,” alisema.
NYERERE SASA!
Akizungumza muandaaji mkuu wa shughuli hiyo, Steve Nyerere alisema wahusika wote walipewa taarifa japokuwa aligawana majukumu na watu wengine kwani asingeweza kuwafikia wote.
“Sisi tuligawana majukumu na nilituma watu kwa wahusika sasa kama hawakuwa na taarifa siyo kosa langu ni la kwao hao niliowapa hilo jukumu, hatukufanya shughuli ile kwa masilahi binafsi zaidi ya kuwakumbuka ndugu zetu,” alisema Steve pasipo kufafanua zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

STYLE KALI:TUMIA HII NDANI YA DAKIKA MOJA TU MWANAMKE AMEKOJOA.

KISIMI (kinembe) kikichezewa mwanamke anaweza kuwataja maawara zake wote.