Katiba ya Tanganyika ndani ya Tanzania.

WAKATI Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa uwapo wa mfumo wa Serikali tatu, Bunge Maalumu la Katiba limeanza kujadili baadhi ya sura ambazo ziliachwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya Katiba ya Tanganyika.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, alisema sura hizo ni pamoja na ile ya Serikali za Mitaa na suala la ardhi.
Kwa mujibu wa iliyokuwa Tume ya Warioba, maeneo hayo yaliachwa kwa ajili ya Serikali   ya Tanganyika. Sitta alisema kuwa suala la Serikali za Mitaa liliwasilishwa kwenye Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, ambaye alilitoa kwa wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).
Alisema waziri huyo aliwasilisha andiko la Jaji Warioba kuhusu ardhi, maliasili na rasilimali za taifa lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya Katiba ya Tanganyika.
“Tumechukua hayo ya tume ili kuendelea kuiboresha rasimu yetu hii tuliyonayo,” alisema.
Alisema kuwa pendekezo jingine kutoka kwa wajumbe wa Bunge hilo ni malengo ya maendeleo, uchumi na jamii.
“Tunataka Serikali isione kuwa kazi yake ni kuongoza watu tu, wajue kwamba wanatakiwa kuhakikisha wanawaendeleza watu kiuchumi,” alisema Sitta.
sitta
Katika hatua nyingine, alisema kuwa Kamati ya Uongozi imeunda kamati ndogo ya watu 10 kupitia suala la Mahakama ya Kadhi, uraia pacha na muundo wa Bunge.
Alisema kuwa kamati hiyo inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu na ina wajumbe watano kutoka Zanzibar na watano kutoka Bara.
Sitta alisema kuwa kamati zote zinatarajiwa kumaliza kazi zake Agosti 27, na Septemba 2 wajumbe wataanza kujadili sura zote.
Alisema pamoja na hali hiyo, wajumbe wamependekeza Katiba mpya itambue haki za walaji ili iwapo mtu akinunua kitu kibovu imlinde.
“Baada ya kazi ya Bunge kwisha, tutakuwa na Katiba bora Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara, Katiba ya viwango kabisa,” alisema Sitta.

Comments

Popular posts from this blog

STYLE KALI:TUMIA HII NDANI YA DAKIKA MOJA TU MWANAMKE AMEKOJOA.

KISIMI (kinembe) kikichezewa mwanamke anaweza kuwataja maawara zake wote.