BABA AMZALILISHA BINTI YAKE KIMAUMBILE.
Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia bado vinaendelea Zanzibar baada ya watu wawili kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kubaka.
Katika
tukio lililotokea Agosti 4, mwaka huu Muhammed Khafidh Thabit (50),
anadaiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14.
Mtuhumiwa huyo alimuingilia binti yake huyo kinyume na maumbile na kumsababishia madhara makubwa mwilini wake.
Akizungumzia
kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,
Mkadam Khamis Mkadam, alisema tukio hilo limetokea eneo la Misufini.
Alisema
baada ya kuhojiwa mtoto huyo, alisema baba yake alikuwa akimlazimisha
kufanya mapenzi baada ya mama yake kutengana na baba huyo.
Alisema uchunguzi wa kidaktari umeonesha kuwa mtoto huyo ameingiliwa mbele na nyuma.
Katika
tukio lingine la mkoa wa Kusini Unguja Polisi inamshikilia Ali Hashim
Ali (27) mkazi wa Mwera visiwani hapa kwa tuhuma za kumuingilia mtoto
wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.
Kamanda
wa polisi mkoani humo, Juma Said Khamis alisema kijana huyo alimrubuni
mtoto huyo kwa kumuahidi kuwa atampatia mbuzi wa kufuga.
Alisema mtuhumiwa huyo alimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika boma la nyumba na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.
Alisema mtuhumiwa ameshawahi kuwalawiti watoto wengine wawili wa kiume.
Watuhumiwa wote wapo chini ya ulinzi.
Akihutubia Baraza la Idi hivi karibuni, Dk Ali Muhammed Shein alikemea vitendo vya udhalilishaji na kutaka vipigwe vita.
Alisema
takwimu za vitendo vya udhalilishaji zinaonesha kuendelea kuwepo kwa
vitendo hivyo licha ya jitihada zinazochukuliwa na serikali na
kushiriana na wanaharakati.
Comments
Post a Comment