Nyumba ya maajabu yazua mapya mjini Tanga.
- Get link
- X
- Other Apps
Kutana na nyumba ya maajabu Tanga ambayo watu wameshindwa kuishi ndani yake

Pengine umeshawahi kusikia stori kadhaa ambazo zinahusisha mkoa wa Tanga na maajabu yake, kuna ambayo nilishawahi kuisikia Tanga kuna wakati ukikipiga teke kifuu eti kinakusemesha kukwambia ukirudishe ulikokitoa.
Sasa Hekaheka ya Leo Aug 21 ni kutokea Tanga na inahusisha nyumba ambayo inasemekana watu wameshindwa kuishi kutokana na maajabu yaliyopo kwamba unaweza kulala peke yako halafu ukiamka unakuta umelala na paka.
Wapangaji kadhaa wameshindwa kuishi na mwenye nyumba katangaza kuuza lakini bado hajapata mteja, unaambiwa walinzi wa nyumba hiyo taa za usiku wanawasha mchana kwa kuhofia likiingia giza watakutana na mambo hayo.
Gea Habib kazungumza hadi na mlinzi aliyewahi kufanya kazi kwenye nyumba hiyo akizungumzia mazingira hayo magumu aliyowahi kukutana nayo ya kazi kwenye nyumba hiyo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment