15 kuuawa katika shambulio Ukraine
Imedaiwa kuwa hakuna
aliyenusurika katika shambulio la msafara wa wakimbizi katika mji wa
Luhansk eneo lililo mashariki mwa Ukraine Jumatatu, taarifa ya waasi
imeiambia BBC.
Taarifa za shambulio hilo bado hazijawekwa wazi
lakini msemaji wa jeshi la Ukraine amesema miili ya watu 15 imepatikana
kutokana eneo la tukio.
Ukraine imewashutumu waasi
wanaoungwa mkono na Urusi kwa kuushambulia msafara wa wakimbizi lakini
wamekana kuhusika na shambulio hilo.
Wakati huo huo, mapigano makali yameripotiwa katikati ya mji wa Luhansk.
Serikali ya Ukraine imesema Jumamne kuwa
mapigano ya mtaani yalikuwa yakiendelea na afisa katika wizara ya mambo
ya ndani ameliambia shirika la habari la Ukraine, Interfax kuwa jeshi
limekuwa likikomboa mji "Kipande kwa kipande".
Imeripotiwa kuwa katikati ya mji wa Luhansk kumekuwa na mashambulio ya risasi usiku wa Jumatatu.
Maelfu ya watu wameukimbia mji wa Luhansk, mmoja
kati ya miji mikubwa miwili inayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na
Urusi, wakati ambapo majeshi ya serikali ya Ukraine yanasonga mbele
kuikomboa miji hiyo.
Mapigano pia yamekwamisha juhudi za kutafuta
miili ya watu katika eneo la tukio kufuatia shambulio la Jumatatu usiku,
katika barabara kati ya ya miji ya Novosvitlivka na Khryashchuvatye.
Zaidi ya watu 300,000 wamekimbia mapigano mashariki mwa Ukraine
Comments
Post a Comment