MAREKANI BADO INAENDELEZA MASHAMBULIZI NCHINI IRAQ, JE KWANINI?
Majeshi ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State huko Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo kaskazini mwa Iraq.
Majeshi ya Marekani kwa ushirikiano na ndege zisizikuwa na marubani zilifanya mashambulizi 14 usiku wa kuamkia leo.
Mashambulizi kumi na manne ya angani yamefanyika katika eneo karibu na bwawa la Mosul na yalilenga kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na wa kikurdi.
Comments
Post a Comment